Molina amejiuzulu ikiwa imepita
saa chache tangu bunge la nchi hiyo kumuondolea kinga ya kutoshtakiwa na sasa
atakabiliana na madai ya rushwa
yanayomuandama ya ubadhirifu wa mamilioni ya dola za huduma za forodha.
Jaji aliyeamuru molina akamatwe
amesema amefanya hivyo kwa kuzingatia katiba ya nchi hiyo ambapo pia ameagiza
katika kipindi ambacho vyombo vya ulinzi nchini humo vikifanya mchakato wa
kumkamata haruhusiwi kutoka nje ya nchi hiyo.
Tayari molina
ambaye muhula wake wa uongozi ulikuwa ukimalizika mwezi januari mwakani
amesema atatii mambo yote atakayoambiwa afanye na vyombo vya sheria katika nchi
hiyo ya Hungary ambapo kujiuzulu kwake pia kulichangiwa na maandamano ya wakazi
wa nchi hiyo waliokuwa wakimpinga.


0 comments:
Post a Comment