Image
Image

Sumaye :Sina muda kwa sasa kumjibu Dr.Slaa bali nawasha moto wa mabadiliko.


Meneja wa kampeni wa vyama vinavyounda umoja wa katiba(UKAWA) na waziri mkuu mstaafu wa serikali ya CCM ya awamu ya tatu BW FREDERICK TLUWAY SUMAYE amewataka watanzania kupuuza tuhuma za ufisadi zilizotolewa na aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA Dr.Wilborad Slaa dhidi ya mgombea urais wa UKAWA Bw. Edward Lowassa pamoja na yeye na kueleza kwamba hawatapoteza muda wa kumjibu kwani hizo ni hila zilizopangwa kutaka kufifisha mabadiliko wanayohitaji  kwa watanzania
Bw.Sumaye ametoa kauli hizo saa chache baada ya kuwasili kwenye uwanja mdogo wa ndege wa Haydom na kuzindua kampeni ya ubunge kwa jimbo la Hanang mkoani Manyara kwa kuwanadi wagombea udiwani na ubunge wa UKAWA kabla ya kuanza kutembelea ngome za CCM,huku akiwataka wananchi kumuunga mkono mgombea wa urais wa ukawa na wagombea viti vya ubunge na udiwani wa ukawa ili kuunda serikali imara itakayowaletea mabadiliko wananchi katika huduma za jamii.
Hata hivyo bw sumaye akimnadi mgombea ubunge wa chadema Bw. Magoma Derick Magoma na madiwani wake Bw.Sumaye amewataka wapigakura kuwachagua wagombea hao ambao watapambana na kero za rushwa,maji ,barabara vijijini na elimu hasa kuondokana na wanafunzi kukaa juu ya mawe ambazo hazijatatuliwa kwa miaka 10,mgombea ubunge huyo akiahidi kurejesha mashamba ya shirika la taifa la chakula kwa wananchi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment