Mbabe wa kivita wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo BOSCO NTAGANDA leo anafikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya ICC kwa mashtaka ya uhalifu wa kivita na dhidi ya binadamu.
Amekanusha mashtaka yote yanayomkabili yakiwemo ya mauaji, ubakaji na kuajiri askari
watoto na zaidi ya waathirika 2,000 wakiwemo watoto askari wa zamani wataitwa kama
mashahidi.
Jenerali NTAGANDA alipigana katika makundi tofauti ya waasi pamoja na jeshi la Kongo na
anatuhumiwa kuwaua raia wapatao 800 wakati wa mashambulio tofauti katika vijiji vya
jimbo la Ituri kati ya mwaka 2002 na 2003.
Pia anashtakiwa kuwabaka wasichana askari na kuwaweka kama watumwa wa ngono.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment