Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Ppa Francis ameanza
ziara yake nchini Marekani. Papa Francis alipokelewa na rais Barrack Obama na
katika ziara yake nchini humo atakuwa jijini Washington DC, New York na
Philadelphia.
Akiwa Marekani, kiongozi huyo wa Kanisa katoliki atakutana na wamini wa
Kanisa hilo, atahotubia pia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kuzungumzia
maswala yanayoikumba dunia ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa na machafuko
yanayoendelea katika nchi mbalimbali.
Ni kwa mara ya kwanza kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki kufanya ziara nchini
Marekani.
Papa alitamatisha ziara yake ya masaa 72 Jumanne wiki hii nchini Cuba
(kisiwa cha kikomunisti), nchi ambayo ilifufua hivi karibuni uhusiano wake na
Marekani kwa mchango mkubwa wa msuluhishi kutoka Vatican na Papa kutoka
Argentina.
Papa Francis alipokelewa na kusherehekewa kwa muda wa siku nne katika mji wa
Santiago nchini Cuba, ambapo kunapatikana bandari kubwa ya kisiwa hicho,
kulikoanzishwa harakati za ukombozi wa Cuba, karibu na kambi ya majeshi ya
Marekani ya Guantanamo.
Papa mwenye umri wa miaka 78 sasa, alisherehekea Misa ya mwisho ya ziara
yake katika mahali patakatifu pa Bikira "del Cobre", katika milima ya
kijani karibu na mji, na ambapo siku moja kabla aliongoza maombi kwa
mustakabali wa watu wa Cuba.
0 comments:
Post a Comment