Nchini Burkina Faso, vikosi vya jeshi vinavyounga mkono
serikali ya mpito na afisa wa wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Rais (RSP)
wamesaini mkataba wa kutoshambuliana usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano.
Wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Raisa (RSP) wamekubali kurudi kambini na
vikosi vya jeshi vinavyounga mkono serikali ya mpito kurudi nyuma kilomita 50
karibu na mji mkuu.
Hata hivyo wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Rais hawakuweka chini silaha
kama ilivyokua imeombwa na vikosi vya jeshi vinavyounga mkono serikali ya
mpito. Mapema Jumanne jioni, jenerali Diendéré alihakikisha kuwa Michel Kafando
ataachiliwa huru rasmi leo Jumatano.
Makubaliano hayo yamesainiwa Usiku wa Jumanne mjini Ouagadougou kati ya
vikosi vya jeshi vinavyounga mkono serikali ya mpito na wanajeshi wa kikosi cha
ulinzi wa Raiswaliofanya mapinduzi. Ni makubaliano ya kuepusha machafuko ambayo
yanaeleza kwamba kikosi cha ulinzi wa Rais (RSP) kinachoongozwa na jenerali
Diendéré kitasalia kambini katika kambi yake wakati ambapo vikosi vya jeshi
vinavyounga mkono serikali ya mpito vitarudi nyuma kilomita hamsini na mji
mkuu.
Makubaliano hayo yamesaini rasmi mbele ya Mogho Naba, Mfalme wa jamii ya
Mossi na kiongozi wa kiroho nchini Burkina Faso. Makubaliano hayo yalitiliwa
saini na Korogho Abdulaziz, Kaimu mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Rais (RSP), na
maafisa wanne waliotumwa na vikosi vya jeshi vinavyounga mkono serikali ya
mpito. Baadhi ya viongozi wa wakuu wa vikosi vya jeshi vinavyouunga mkono
serikali ya mpito ambao walianzisha jitihada ya kuelekea katika mji mkuu wa
Burkina Faso, Ouagadougou ni wanafahamiana na wale wa kikosi cha ulinzi wa Rais
(RSP).
Wakati huo huo ujumbe wa ECOWAS unaoundwa na marais kutoka jumuiya hiyo,
unatarajia kuwasili mjini Ouagadougou ili kuendelea na mashauriano kati ya
pande hizo mbili na kujadili kuhusu kumrejesha mamlakani Rais Michel Kafando na
taasisi zingine za mpito.
0 comments:
Post a Comment