Rais wa Congo Brazaville Denis Sassou Nguesso ametangaza
kuwa kutafanyika kura ya maoni kubaidlisha Katiba ya nchi hiyo.
Ngueso ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 31 sasa amesema tume ya
kushughulikia marekebisho ya katiba itateuliwa na kupendekeza marekebisho
yanayohitajika kabla ya tarehe ya kura hiyo ya maoni kutangazwa rasmi.
Hii inaamanisha kuwa ikiwa kura hiyo itafanyika, rais huyo mwenye umri wa
miaka 71 huenda akawania tena urais kwa muhula mwingine mwaka ujao.
Katiba ya sasa hamruhusu rais Denis Sassou Nguesso kuwania tena urais na
wanasiasa wa upinzani wamekuwa wakipinga kubadilishwa kwa katiba kumpa nafasi
nyngine ya kuongoza taifa hilo la Afrika ya Kati.
0 comments:
Post a Comment