Baada ya miezi sita ya uhamishoni nchini Saudi Arabia, Rais
wa Yemen Abd Rabbo Mansour Hadi amerejea Jumanne wiki hii katika mji wa Aden,
mji mkuu wa kusini, uliyotangazwa mji mkuu wa "muda", ambapo
kunapangwa mashambulizi kwa minajili ya udhibiti wa eneo la kaskazini mwa nchi
linaloshikiliwa hadi sasa na waasi wa Kishia.
Hadi alikimbilia katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh, baada ya
kulazimishwa kuondoka mji wa Aden Machi 25, ambako alikimbilia kutokana na
kusonga mbele kwa waasi wa Kishia wa Huthi, ambao wameendelea kuudhibiti mji
mkuu Sanaa na sehemu kubwa ya nchi ya Yemen.
Hadi meahidi Jumanne usiku kurudi haraka katika mji wa Sanaa. "Kurudi
katika mji mkuu wa Sanaa ni hivi karibuni, baada ya ukombozi wa miji yote na
majimbo yanayoshikiliwa na wanamgambo waliofanya mapinduzi ", amesema
katika taarifa fupi iliyochapishwa na shirika la habari la serikali la Saba.
Kurudi kwake, siku mbili kabla ya Eid al-Adha, Sikukuu ya Kiislam,
kunafuatia kurudi kwa Makamu Rais Khaled Bahah na mawaziri kadhaa wiki
iliyopita katika mji wa Aden uliyodhibitiwa kutoka mikononi mwa waasi wa Kishia
wa Huthi mwezi Julai mwaka 2015.
Rais Hadi, anayetambuliwa na jumuiya ya kimataifa, alisafirishwa katika mji
wa Aden na ndege ya kijeshi ya Saudi Arabia ambayo ilitua kwa siri katika
mapema jioni katika uwanja mdogo wa ndege karibu na kambi ya keshi mjini Aden,
chanzo cha usalama kimebaini.
Washirika wake kadhaa wa karibu na wajumbe wa serikali waliwasili mjini Aden
kabla yake Jumapili mchana wakiwa katika ndege ya shirika la ndege la Yemenia,
chanzo cha usalama kimeongeza.
Machafuko nchini Yemen yamesababisha vifo vya watu 4,900 na wengine 25,000
waliojeruhiwa tangu mwezi Machi, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
0 comments:
Post a Comment