

Polisi Mkoani Dodoma imepiga marufuku shughuli za vikundi vya ulinzi vyenye mwelekeo wa kijeshi vinavyomilikiwa na vyama vya siasa na kuonya kuwa haitakuwa na mzaha kwa mtu, kikundi au taasisi itakayokiuka katiba katika kipindi cha hiki cha kampeni na baada ya uchaguzi mkuu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME pia amevitaka vyama vya siasa, wafuasi wao na wananchi wa mkoa huo, kuzingatia utii wa sheria katika kipindi chote cha kampeni na baada ya kupiga kura na kutangazwa matokeo na kisha kuapishwa kwa waliochaguliwa.
Katika hatua nyingine, jeshi hilo kwa kushirikiana na Mfuko wa Pensheni wa Serikali - LAPF- limemkamata mtu aliyetambuliwa kwa jina la DAVID MAGESA MAKALI na kumfikisha mahakamani, baada ya kujifanya mtumishi wa TAMISEMI na mifuko ya LAPF, PSPF na ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, kwa kuwatapeli wastaafu Mamilioni ya Shilingi katika mikoa 15 nchini huku akijifanya kuwa yeye ni ofisa wa taasisi hizo anaye shughulikia pensheni.


0 comments:
Post a Comment