Kampeni za uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu nchini Tanzania
zimepamba moto huku kila mgombea akitoa ahadi kubwa na nyingi kwa wapiga
kura.
Uchaguzi wa mwaka huu nchini Tanzania unatarajiwa kuwa na hali
ya kipekee katika kila upande na serikali ya nchi hiyo imesema
imejiandaa vilivyo kulinda usalama.
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema kuwa atafunga kamera maalumu za
CCTV katika miji mikuu ya nchi hiyo kukabiliana na wahalifu nchini humo.
Rais
Kikwete amesema katika hafla ya kuagana na wapiganaji na walinzi wa
usalama wa Tanzania iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,
jijini Dar es Salaam kuwa, Serikali yake inakamilisha mpango wa kufunga
kamera hizo ili kuimarisha ulinzi na usalama wa raia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment