Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA -,JUMA DUNI HAJI amesema, iwapo Watanzania watamchagua mgombea Urais wa chama hicho,EDWARD LOWASSA, serikali itahakikisha barabara zote zinazounganisha wilaya moja na nyingine katika mikoa ya Lindi na Mtwara zinajengwa kwa kiwango cha lami.
Mgombea mwenza huyo ameyasema hayo kwa nyakati tofauti alipokuwa akihutubia mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu iliyofanyika kwenye majimboya Mtama Wilayani Lindi na katika kijiji cha Nanjilinji Kilwa Kusini mkoani lindi.
Amesema mojawapo ya barabara ambazo serikali ya CHADEMA itaijenga kwa kiwango cha lami, ni barabara ya Masasi hadi Liwale, yenye urefu wa Kilomita zaidi ya 120 ili ipitike wakati wote.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA taifa upande wa Zanzibar, SAID ISSA MOHAMED akiwahutubia wananchi wa jimbo la Mtama lindi vijijini amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura tarehe 25 mwezi ujao.
Home
News
CHADEMA:Barabara za Lindi na Mtwara zitajengwa kwa kiwango cha lami LOWASSA akishinda Urais.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment