Barack Obama amehakikishiwa kuwa na uwezo wa kutekeleza
makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran. Ikulu ya Marekani imekwisha pokea
ahadi za kutosha za kuungwa mkono na maseneta, kuweka mbali tishio la kurudisha
nyuma makubaliano hayo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa Rfi katika mji wa Washington,
Anne-Marie Capomaccio, Rais wa Marekani Barack Obama amefanikiwa kupata
uungwaji mkono kutoka kwa Maseneta kuwazuia wale wa Republican kupinga
kupitisha mswada kuhusu mradi wa amani wa nyuklia wa Iran.
Maseneta wa Democratic wameugana kumuunga mkono rais Obama,
uamuzi ambao ni pigo kwa maseneta wa Repblican ambao wameweka wazi kupinga
mktaba huo.
Kupitishwa kwa mktaba huo inamaanisha kuwa Marekani itaondoa
vikwazo vya kuucumi dhidi Iran kama mojawapo ya makubaliano ya utekelezwaji wa
mradi huo wa nyuklia.
Bunge la Congress linatarajiwa kujadili na kuupigia kura
mkataba huo tarehe 17.


0 comments:
Post a Comment