Mashuhuda wanasema mtu wa kujitoa muhanga alijilipua wakati waumini wakitokea msikitini na wapiganaji wa jihadi wa kikundi cha Islamic State wamedai kuhusika na shambulio hilo.
Mapema wafanyakazi wawili wa misaada waliuawa kwa kupigwa risasi, na Chama cha Msalaba Mwekundu kimesema wafanyakazi wake hao wawili wameua wakiwa katika msafara mjini Sanaa.
Inasadikiwa mtu mwenye bunduki alilifyatulia gari lao wakati wanasafiri kupitia jimbo la Kaskazini la Amran, wakati wakitokea Saada, ngome ya waasi wa Houthi.


0 comments:
Post a Comment