Wakulima kutoka wilaya 12 watashiriki katika maandamano hayo
katika eneo la taifa. Ujumbe wa wakulima hao utapokelewa leo mchan katika mji
wa Matignon, na mwingine utakwenda Bungeni ili kufikisha malalamiko yake kwa
wabunge. Maandamano haya yenye ushawishi mkubwa yametajwa kuwa ya kihistoria na
wafugaji wengi.
Wakulima wanaelekea kwanza katika mji wa Paris ili waweze
kutambuliwa. Wanahisi kwamba hawaeleweki na wamekua wakipuuzwa, na raia watambuwe
shida na maisha duni yanayokumba wakulima.
" Kwenda Paris ni pigo kubwa. Kuna matrekta 1500,
kutakuwa na zaidi ya watu elfu 4 hadi elfu 5 mchana huu katika eneo la taifa.
hali hii inaonyesha dhiki, shida ya wakulima. Leo tunahitaji ufumbuzi wa kweli
ambao ni endelevu kwa ajili ya kutupa upya mitazamo na kutupongeza kwa kuamka
asubuhi na kufanya bidhaa bora za kilimo ", amesema Luc Smessaert, makamu
wa rais wa wa Shirikisho la Wakulima nchini Ufaransa (FNSEA).
Viwango
Mzozo huo pia una sababu zaidi ya kiuchumi na kijamii. Bila
shaka, wakulima hawa hawategemei kitu cha ajaabu, lakini wanataka ufumbuzi
katika madai yao. Miongoni mwa madai yao, wanaiomba serikali punguzo la gharama
ya kazi wanaoifanya na gharama za wafanyakazi. Hizo ni moja ya pointi muhimu.
Ufaransa inaendesha shughuli hii ya kiliomo kwa viwango
wakati majirani zake, Ujerumani na Hispania huzalisha kwa nafu na kuuza zaidi
nje.
" Serikali inapaswa kujitoa kwa kimuundo, na
kutupunguzia mzigo wa gharama na kutupunguzia pia viwango vya ilivyoweka. Na
kusema kwamba nafasi kwa Ufaransa ni kuwa na mifugo yenye maziwa, ng'ombe na
nguruwe ", amesisitiza Thierry Roquefeuil, rais wa Shirikisho la kitaifa
la Uzalishaji wa Maziwa.


0 comments:
Post a Comment