Ijumaa wiki hii, Rais wa Marekani Barack Obama amempokea
Rais wa China Xi Jinping katika bustani ya Ikulu ya Marekani, nyimbo za mataifa
hayo mawili zimepigwa, huku mizinga 21 ikirushwa hewani.
Ziara hiyo ya Xi Jinping nchini Marekani inatokea, huku
kukiwa na mvutano kati ya mataifa haya mawili makubwa.
Ziara hii ya kwanza ya kiongozi wa China nchini Washington
tangu kuchukua madaraka inakuja wakati ambapo uchumi wa China unaonyesha dalili
halisi ya kudorora. Ziara hii ya Xi Jinping pia inakuja wakati Marekani imekua
ikiilamu China kufanya udukuzi wa mawasiliano yake.
Serikali ya Marekani ina matumaini ya kuona ushirikiano kati
ya China na Marekani "ukiimarika" katika suala la: mapambano dhidi ya
mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa mujibu wa afisa wa Marekani, China inapaswa kutangaza
Ijumaa wiki hii ikiwa ni pamoja na kuanzishwa mwaka 2017 kwa soko la kiwango
cha gesi ya CO2 inayolenga kutoa bei ya mkaa ya mawe na hivyo kuhamasisha
kupungua kwa uzalishaji wa gesi chafu katika sekta ya viwanda . Nchi
inayozalisha kwa kiwango kikiubwa gesi chafu duniani tayari imefanya majaribio
lakini bado haijaanzisha soko la kitaifa.
Katika mkutano wao mwezi Novemba mwaka 2014, mjini Beijing,
Obama na Xi walitangaza mkataba ambapo waliwasilisha malengo yao katika suala
la uzalishaji wa gesi chafu: kupunguza kutoka 26% hadi 28% ifikapo mwaka 2025
ikilinganishwa na mwaka 2005 kwa Umoja wa Mataifa, sawa na mwaka 2030 kwa
China.
0 comments:
Post a Comment