Serikali ya Kenya imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia Jumatatu huku mgomo wa walimu ukiendelea.
Barua kutoka kwa wizara ya elimu imeagiza shule zote za umma na za kibinafsi zifungwe na wanafunzi warudi nyumbani.
Watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.
Katibu Mkuu wa chama cha walimu nchini humo KNUT ameambia BBC kuwa tayari amepokea barua hiyo ya kufungwa kwa shule kutoka kwa serikali.
Amesema chama hicho kilikuwa kimeishauri serikali ifunge shule “zamani”.
Mahakama inatarajiwa kuamua Ijumaa ijayo iwapo mgomo huo wa walimu, ambao umelemaza masomo muhula wa tatu, ni halali au la.
0 comments:
Post a Comment