Viongozi wote wa CCM wa kata ya mkomazi na pamoja na wapiga
kura 1,400 wa eneo hilo wilayani Korogwe wamejiunga na CHADEMA huku baadhi yao
wakiamua kugombea nafasi mbali mbali za uongozi kwa tiketi ya chama hicho.
Wakizungumza katika mkutano wa kampeni ulifanyika katika
kijiji cha mikocheni kilichopo kata ya mkomazi wilayani Korogwe baadhi ya
viongozi hao pamoja na wengine wa CCM katika kata sita waliokatwa majina yao
katika zoezi la kura za maoni kwa tiketi ya CCM wamesema wameamua
kujiunga na chadema pamoja na wapiga kura wao ili kuongeza nguvu kupata
wawakilishi wa wananchi katika baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Korogwe.
Kwa upande wake katibu wa CHADEMA jimbo la Korogwe Bwana.Salim
Sempoli amemuomba mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi jimbo la Korogwe
kuharakisha malalamiko ya wapiga katika baadhi ya vituo ambapo sehemu kubwa ya
majina ya wapiga kura katika jimbo la Korogwe vijijini hayaonekani na hadi sasa
hakuna utaratibu uliofanywa kusaidia tatizo hilo kwa sababu linaweza kuleta
viashiria vya uvunjifu wa amani wakati wa zoezi la kupiga kura.
Kufuatia hatua hiyo mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema
Emmanuel Kimea amewataka wananchi kuwachagua viongozi wa chama hicho kuanzia
ngazi ya taifa,ubunge na udiwani kwa sababu ndani9 ya chama kikoja changamoto
zinazowakabili katika kata ya mkomazi ikiwemo ya migogoro ya ardhi haiwezi
kumalizika kama hawatafanya mabadiliko.
0 comments:
Post a Comment