Waziri wa Fedha, Saada Mkuya alitoa kauli hiyo
alipokuwa akizungumza kwenye hafla fupi ya makubaliano yaliyofanyika
jijini Dar es Salaam.
Alisema kufanikiwa kwa mradi huo kutasaidia kuongeza ajira kwa
vijana, kuongeza uzalishaji wa chakula na kupunguza idadi ya kuagiza
matrekta kutoka nje ya nchi.
“Serikali ya Tanzania inashukuru Serikali ya Poland kukubali kutoa
mkopo huo ambao utasaidia kuongeza uzalishaji wa chakula katika sekta ya
kilimo na kuondoa matumizi ya jembe la mkono,” alisema.
Mkuya alisema baada ya kusaini mkataba huo, wanaendelea kufanya
maandalizi ya kupokea vifaa mbalimbali vya mradi ili ujenzi wake uanze
mara moja.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, alisema
ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza matrekta nchini utasaidia kuongeza
idadi ya uzalishaji zana hizo za kulimia.
Alisema mradi huo utasaidia harakati za kutokomeza umaskini
uliosababishwa na kilimo cha jembe la mkono ifikapo 2025 kila mkulima
atumie trekta.
Aidha, Wasira alisema mkopo huo utasaidia ujenzi wa maghala ya
kuhifadhia nafaka toka tani 240,000 za sasa na kufikia tani 400,000.
“Naendelea kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo ya Poland, Zofia Szalczyk, kujua lini utekelezaji wa mkataba
utaanza,” alisema.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo wa Poland, Zofia Szalczyk,
alisema serikali yake itaendelea kutoa mkopo kwa Serikali ya Tanzania
ili kuendelea kukuza uhusiano.
0 comments:
Post a Comment