Ofisi
ya Waziri Mkuu nchini Finland imetangaza mpango wake wa kutaka
kupunguza mishahara ya mawaziri kwa aslimia 5.
Serikali
ya Finland ilichapisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2016 siku ya
Jumatatu iliyoonesha kiwango cha fedha Euro bilioni 54.1 zinazotazamiwa kukidhi
mahitaji ya nchi.
Finland
inalenga kuhifadhi fedha Euro milioni 2 kila mwaka kwa kupunguza mishahara
ya mawaziri kwa asilimia 5 kuanzia muhula mpya wa mwaka 2015-2019.
Vile
vile, mawaziri wote watatakiwa kufanya kazi bila malipo kwa wiki moja
kila mwaka.
Maelezo
zaidi ya ofisi ya waziri mkuu yamearifu kwamba utaratibu huo mpya pia
utawekewa makatibu wa wizara na wasaidizi wao.
Kwa
sasa mawaziri wa Finland hupokea mshahara wa fedha Euro 9,788
huku waziri mkuu akilipwa Euro 11,742 kwa mwezi.
Hapo
awali, waziri mkuu Juha Sipila aliwahi kupunguza idadi ya wizara kutoka 19 hadi
14 na ofisi za makatibu kutoka 9 hadi 4 kama mojawapo ya hatua za kupunguza
matumizi ya fedha nchini serikalini.
0 comments:
Post a Comment