Mgombea
urais kupitia chama cha ACT wazalendo Anna Mghwira ameahidi kuwa chama chake
kitahakikisha raslimali zote zinazopatikana katika kila mkoa zinatambulika
kikatiba ili wananchi wawe na uwezo wa kuhoji na kuzitumia kuboresha huduma
katika mkoa husika.
Kauli
hiyo ameitoa wakati akihutubia wananchi katika viwanja vya mashujaa mjini
mtwara,ambapo amesema kuwa serikali yake itahakikisha mkoa wa mtwara unanufaika
na raslimali ya gesi sambamba na mazao ya kilimo yanayolimwa kwa wingi ili
wananchi waweze kunufaika na ukuzaji wa uchumi katika maeneo yao.
Mh.Mghwira
mapema akiwa katika wilaya ya newala,katika kijiji cha mnyambe jimbo la newala
vijijini,ameelezwa na mgombea ubunge wa chama hicho Pilila Lawi Sijaona kuwa
wilaya hiyo ina tatizo kubwa la maji licha ya kuwa na vyanzo kadhaa,ambapo
ameahidi kumaliza tatizo hilo mara tu atakapopata ridhaa huku mgombea mwenza wa
urais Hamad Yusuf akieleza kuwa ACT wazalendo itapanua na kuboresha
bandari ya mtwara ili kupunguza msongamano katika bandari ya Dar es Salaam.
Tayari
mgombea urais wa ACT anna mghwira amekwishatembelea mikoa 13 kuomba kura.
0 comments:
Post a Comment