Shirika la Hisani la Madaktari Wasiokuwa na Mipaka limetaka kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Surua katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao umeua watu 320 na kuambukiza wengine Elfu-30.
Mratibu wa shirika hilokatika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Dakta MICHEL JANSSENS ameonya kuwa janga la afya litaikumba nchi hiyo iwapo ugonjwa huo unaoenea kwa kasi katika jimbo la Katanga hautazuiliwa ndani ya siku 60 zijazo.
Amesema hatua ya haraka inahitajiwa kuchukuliwa sasa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo kwani itakuwa vigumu kuwafikia wagonjwa wakati wa msimu wa mvua unaotarajia kuanza ndani ya miezi miwili.
Mwezi uliopita Umoja wa Mataifa ulitoa Dola Milioni 2 na Laki-4 kusaidia serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na makundi mengine ya kibinadamu kusaidia kukabiliana na mlipuko huo.
Lakini shirika hilo linasema fedha peke yake haitoshi bali watendaji zaidi kwenye uwanja wa mapambano ambapo hadi sasa ni shirika hilo pekee linalotibu na kuchanja watoto.
Home
Afya
Shirika la Hisani la Madaktari Wasiokuwa na Mipaka limetaka kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Surua.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment