Image
Image

UKAWA:Mnyimeni Magufuli kura kutokana na kuvunja nyumba za wananchi maskini.


Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya chama cha Demokrsia na maendeleo ( CHADEMA ), anayewakilisha vyama vinne washirika vya umoja wa katiba ya wananchi ( UKAWA ) Mh. Juma Duni Haji amewataka watanzania kumnyima kura mgombea wa chama cha mapinduzi ( CCM ), Dk.John Pombe Magufuli kutokana na kuvunja nyumba za wananchi maskini,kauli za kejeli kwa wananchi wa kigamboni na kuhusika na uuzaji holela wa nyumba za serikali kwa bei ya kutupa.

Mh.Duni Juma Haji ametoa mwito huo kwa watanzania katika nyakati tofauti wakati akihutubia mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu kwa wananchi wa wilaya za Rufiji, Mkuranga na Kisarawe mkoani Pwani na kuongeza kuwa anazidi kushangazwa na kauli ya hivi karibuni ambayo mgombea urais huyo wa CCM DK. JOHN POMBE MAGUFULI ameitoa akiwa mkoani Mtwara ya kuwataka askari polisi kuwaua majambazi huku akihoji ni vipi serikali ya CCM chini ya rais Jakaya Kikwete imeshindwa kupambana na wezi wa fedha za Umma.

Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam ambaye kwa sasa ni kada wa Chadema John Guninita naye akapanda jukwaani kumzungumzia  mgombea urais wa chama cha mapinduzi dk.John Pombe Magufuli.

Aidha mgombea mwenza huyo wa urais kupitia ukawa,akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu katika jimbo la Kisarawe uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Chanzige,Mh.Juma duni Haji amewaomba wananchi kumchagua mgombea ubunge wa jimbo hilo anayetokana na chama cha wananchi CUF Rashid Mwinshehe Mzange, maarufu kama Kingwendu kwa jina la usanii na alipopandishwa jukwaani ili kuomba kura.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment