Davutoglu atoa tangazo linalozumgumzia hali ya wahamiaji wanaoingia barani Ulaya.
Waziri Ahmet Davutoglu ametoa wito kwa serikali na viongozi wa Ulaya akiwataka kuingiliakati vilivyo suala la wahamiaji kabla ya mambo hayajaharibika.
Davutoglu alisema kuwa machafuko ya muda mrefu Mashariki ya Kati yanayopewa kisogo yamepiga hodi barani Ulaya.
Baada ya kuokotwa kwa muili wa mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitatu katika pwani ya bahari inaashiria mateso ya muda mrefu na kutoa wito wa mshikamano kwa ulimwengu mzima.
Davutoglu ameishtumu Ulaya kwakufanya mikutano isiotoa matunda katika suala la wahamiaji.
Davutoglu alizidi kufahamisha kuwa jumuia ya kimataifa inayodai kuwakilisha ulimwengu na kusemakuwa Uturuki imekuwa ikiwapa hifadhi kwa muda mrefu na kuwa na idadi kubwa ya wakimbizi duniani.
Waziri Ahmet Davutoglu alimalizia akifahamisha kuwa maelfu ya Aylan wamezaliwa katika ardhi ya Uturuki na Uturuki itaendelea kuwapokea wahamiaji kutoka Syria, Iraq na kungineko bila ya kujali tamaduni zao na hilo Umoja wa Mataifa unatosha kuwa shahidi.


0 comments:
Post a Comment