Image
Image

Wananchi watakiwa kujiandaa kudhibiti maafa yanayo weza kujitokeza.

Ofisi ya Waziri Mkuu imewashauri wananchi wakiwemo wadau wa maendeleo, kushiriki kwa ukamilifu kudhibiti na kujiandaa kuzuia maafa yanayo weza kujitokeza kwa taifa pamoja na athari zake ili kuondoa vifo na matatizo yanayoepukika  badala ya jukumu hilo kuiachia Serikali pekee.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia-Jenerali  MBAZI MSUYA wakati wa uzinduzi wa mpango wa kujiandaa kukabiliana na maafa na zoezi la majaribio kwa halmashauri za Wilaya za Kilosa na Mvomero Mkoani Morogoro.
Ametaja aina ya majanga yanayojitokeza au kulikumba taifa kuwa ni pamoja na mafuriko, milipuko ya mabomu na  ugonjwa wa Kipindupindu.
Kaimu  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,  NOELI KAZIMOTO amesema Watanzania wanapaswa kujipanga kwa matatizo ya maafa kwa muda wowote kwani hutokea ghafla bila taarifa.
Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa inayokabiliwa na majanga ya mafuriko na Kipindupindu mara kwa mara, mambo ambayo yanahitaji jitihada za pamoja katika kudhibiti na kukabiliana na hali hiyo ili kutoleta athari zaidi kwa jamii.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment