Mkataba huo wa miaka mitano wa fedha dola milioni 5 utawezesha
mechi za ligi kuu ya soka ya Zambia kuonyesha katika televisheni ya Supersport
hadi mwaka 2020.
FAZ ilitoa maelezo na kusema kwamba hatua hiyo itasaidia kukuza
soka nchini Zambia kutambulisha ligi yao kimataifa.
Mwenyekiti wa FAZ Kalusha
Bwalya, alisema kwamba mkataba huo wa miaka mitano pia utahakikishia Zambia
fursa mpya za kibiashara za kimataifa zinazohusiana na michezo.


0 comments:
Post a Comment