Image
Image

Wenger - umnunua Martial kwa gharama ya juu ni ishara ya upungufu wa wachezaji wazuri kwenye soko.


Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger, ambaye amekashifiwa vikali na mashabiki pamoja na wachambuzi wa soka kwa kutowasajili wachezaji wapya, amemkejeli kocha wa Manchester united Louis van Gaal ambaye alitumia kitita kikubwa cha fedha kumsajili mchezaji mwenye miaka 19.
Anthony Martial alisajiliwa kwa gharama ya Yuro milioni 38 kutoka Monaco ambako alifunga mabao 15 katika mechi 70 alizocheza. Kwa wengi ni mchezaji mchanga asiyetambulika.
Huenda Wenger alikuwa na uhasama wa kibinafsi kwani Martial alihusishwa katika kikosi cha Monaco kilichoinyuka Arsenal kwa mabao 3 kwa 1 katika mechi ya ligi ya mabingwa wa Ulaya msimu uliopita.
Wenger alishutumiwa vikali kwa kutomsajili mshambuliaji licha ya kuona wazi kuwa timu yake ilihitaji kuboreshwa katika safu ya washambuliaji. Wenger anaendelea kuweka matumaini yake katika Olivier Giroud ambaye alikashifiwa na mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo Thierry Henry.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment