Watu 20 wameuawa na wengine 140 wamejeruhiwa katika mashambulio mawili ya mabomu Kaskazini mwa Cameroon.
Milipuko
hiyo ilitokea jimbo la Kerawa ambako jeshi la Cameroon limekuwa
linapambana na wapiganaji wa Nigeria wa kikundi cha Boko Haram.
Hivi
karibuni kumekuwa na wimbi la mashambulio kaskazini mwa Cameroon
yanayolaumiwa kufanywa na wapiganaji wa Jihadi wa kikundi hicho cha Boko
Haram.
Mlipuko wa bomu la kwanza ulitokea kwenye soko la Kerawa na
wa pili baadaye kiasi cha mita 200 kutoka kambi ya jeshi la nchi kavu na
baadhi ya taarifa zinasema watu wapatao 30 wameuawa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)



0 comments:
Post a Comment