Mkurugenzi mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini - TCRA- ameridhishwa na utendaji unaofuata maadili ya utangazaji katika vyombo vya habari vya IPP.
Mkurugenzi huyo Dakta ALLY YAHAYA SIMBA ameyasema hayo baada ya ziara yake kwenye vyombo vya habari vya utangazaji vya IPP.
Akiongozwa na mkurugenzi mtendaji wa ITV Radio One, JOYCE MHAVILLE, alipata fursa kutembelea studio za EATV//EA Radio, Capital Radio na Radio One, nakupatiwa maelezo ya kina ya namna vituo vinavyofanya kazi kwa kuzingatia ueledi kanuni na sheria za utangazaji zilizowekwa na TCRA.
Dakta ALLI aliyefuatana na maafisa kadhaa kutoka TCRA, alipata fursa pia kutembelea studio za kidijitali za ITV, na kujionea namna ambavyo zinafanya kazi kisasa ikiwa ni pamoja na zile zinazotumia mfumo wa 3d, pia akipata ufafanuzi wa namna chumba cha habari cha ITV kinavyofanyakazi zake za kila siku.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ITV /Radio One JOYCE MHAVILE amemhakikishia mkurugenzi huyo kuwa vituo hivyo vitaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuuhabarisha umma kwa kufuata kanuni na maadili yaliyokwisha kuwekwa na TCRA.
0 comments:
Post a Comment