Rais SALVA KIIR wa Sudan ya Kusini leo anatarajia kuhutubia taifa lake kuhusu mkataba wa amani aliotia saini hivi karibuni pamoja na kiongozi wa waasi Bwana RIEK MACHAR.
Katika hotuba yake hiyo msemaji wake ameeleza kuwa Rais KIIR atawaambia raia wa nchi
hiyo kuunga mkono utekelezaji kikamilifu wa mkataba huo wa amani ya kudumu nchini humo.
Msemaji huyo Bwana ATEN WEK ATEN amesema rais huyo pia atazungumzia kuhusu uchumi wa nchi hiyo na umuhimu wa kuponya makovu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa maridhiano.
Mkataba wa kumaliza karibu miezi ishirini ya mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo ulitiwa
saini mwezi uliopita huku Umoja wa Mataifa ukionya kuchukua vikwazo dhidi ya wale ambao
watakiuka utekelezaji wake.
0 comments:
Post a Comment