Wanawake wa mkoa wa Singinda wamelalamikia wafanyabiashara kununua mazao yakiwa mashambani kwa rumbesa kwa bei wanayoitaka hali inayowaumiza kutokana na kulima kwa hasara na hivyo kuwataka wagombea waje na majibu jinsi ya kuwasaidia kupata masoko.
Wanawake hao wamesema wanashindwa kupata faida katika mazao wanayolima ikiwemo Alizeti na viazi ambavyo wachuuzi hununua mazao yakiwa shambani huku wakitupia lawama wamiliki binafsi wa viwanda vidogovidogo vya kukamua alizeti kuzidi kuwakandamiza wakulima wa zao hilo.
Kwa Upande wake mke wa mgombea urais kupitia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), mama Regina Lowassa akizungumza na wanawake hao amewataka kutokukata tamaa na wasikubali kudanganyika na badala yake wachague viongozi watakaopigania haki kuhakikisha wanasimamia serikali ipeleke viwanda ili kupunguza mzigo kwa wanawake.
Bi. Regina ameongeza kuwa imefika wakati sasa kwa akinamama wajasiriamali hasa wa kilimo kupata faida ya wanachokitengeneza na changamoto hizo zote zitaondolewa au kupunguzwa kwa kiasi kikubwa na serikali ya Ukawa.
0 comments:
Post a Comment