Waziri wa ugatuzi Kenya Anne
Waiguru kwa siku kadha sasa amekuwa mada ya jumbe kwenye mitandao ya
kijamii nchini humo na hasa Twitter, wengi wakitaka Rais Uhuru Kenyatta
amsimamishe kazi.
Ni nini sababu ya kuvuma kwa jina lake
mtandaoni? Yote yalianza kutokana na tangazo lake Ijumaa kwamba
amewasilisha majina ya maafisa 21 wakuu kutoka wizara yake na Shirika la
Vijana wa Huduma kwa Taifa wachukuliwe hatua.
Hii ni baada ya afisi ya uchunguzi wa jinai kupendekeza washtakiwe kwa tuhuma za kula njama ya kulaghai NYS.
Bi
Waiguru alisema uchunguzi umebaini Sh791 milioni zilitoweka kutoka kwa
shirika hilo kupitia malipo ya kutiliwa shaka kwa kampuni za kibinafsi.
Wapinzani
wa serikali ya Rais Kenyatta walichukua nafasi hiyo kukosoa juhudi zake
za kupambana na ufisadi na kumtuhumu kumpendelea waziri huyo.
Kiongozi
wa upinzani Raila Odinga katika mkutano wa kisiasa mtaa wa Kibera,
Nairobi Jumapili alisema ndiye aliyekuwa wa kwanza kufichua kuhusu
kashfa hiyo, na tangazo la Bi Waiguru lilionyesha kwamba alikuwa sahihi
na kudai waziri huyo anakingwa na Rais Kenyatta.
Wakenya kwenye
Twitter wamekuwa wakitumia vitambulishi mbalimbali kumtaka Bi Waiguru
kujiuzulu, baadhi vikiwa #WhyWaiguruMustGo na #SuspendWaiguru.
"Ili
kushinda vita dhidi ya ufisadi, hatufai kupendelea,” mmoja aliandika.
"Huwezi kuruhusu wadogo wako waibe pesa kisha udai huna hatia. Lazima
kuna pesa zilifika karibu naye,” aliandika mwingine.
Wanaomuunga mkono pia hawajaachwa nyuma, wakitumia vitambulisho vivyo hivyo kumtetea.
"Ufasaha,
utendakazi mwema na ujasiri ni baadhi ya sababu ambazo zitamfanya
Waiguru asiende popote,” mmoja wao aliandika. "Yeye ni mzalendo kamili
na kiongozi mwanamke. Lazima tumuunge mkono,” ameongeza mwingine.
0 comments:
Post a Comment