Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limebaini
kuwepo kwa vitendo vyaa wanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania kujihusisha na
masuala ya Siasa wakiwa katika mavazi rasmi ya mpira ambayo yana nembo za
vilabu na wadhamini wa Ligi.
Katiba ya TFF ibara ya I (4) inatamka “TFF is
neutral in matters of politics and religion. Discrimination of any kind
against a country, private person or group of people on account race, skin
colour, ethnic, national or social origin, gender, language, religion,
political opinion or any other opinion, wealth, birth or any other status is
strictly prohibited and punishable by suspension or expulsion.”
Aidha kanuni za Ligi, Kanuni ya 14(40) inatamka: “
Hairuhusiwi kwa mchezaji, mwamuzi au kiongozi wa timu kuonyesha kwa njia
yeyote tangazo au ujumbe unaohusiana na dini yeyote au ulio na madhumuni
maalum bila idhini ya TFF/TPLB”.
TFF inachukua fursa kuwakumbusha wana familia wote
wa mpira wakiwemo viongozi, wachezaji, waamuzi, makocha na madaktari wa
michezo kuwa ni marufuku kuelezea hisia zao za kisiasa au kujihusisha katika
kampeni za kisiasa wakiwa katika mavazi rasmi ya mpira zikiwemo jezi na track
suites zenye nembo za TFF, vilabu wadhamini na ligi, Taifa stars au za
washirika wa TFF wakiwemo wadhamini.
Aidha ni marufuku kwa mashabiki wa mpira kutumia
fursa ya mechi za mpira wa miguu kubeba mabango au kusambaza ujumbe wa
kisiasa.
Hatua kali zitachukuliwa kwa wataokiuka mahitaji
ya katiba na kanuni za mashindano. TFF inatambua haki za wanamichezo
kushiriki katika siasa ili mradi ushiriki wao hazikiuki kanuni na mahitaji ya
katiba za TFF na FIFA.
|
0 comments:
Post a Comment