Juma Nyoso akifanya tukio la udhalilishaji dhidi ya John Bocco msimu huu wa ligi kuu Tanzania.
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi,
amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mchezaji Juma Nyoso,
baada ya kufanya udhalilishaji kwa kumshika makalio mchezaji wa timu ya
Azam, John Bocco ‘Adebayor’.
Kauli hiyo ya Malinzi aliitoa kupitia katika mtandao wa kijamii
kwenye akaunti yake ya Twitter, ambapo alisema mchezaji huyo aliyefanya
kitendo hicho, atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Alisema ni kitendo cha ajabu ambacho hakiwezi kufumbiwa macho kitachukuliwa hatua ili kisijirudie tena.
“Lazima hatua kali zichukuliwe dhidi ya mchezaji huyo ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia hizi,” alisema Malinzi.
Katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliofanyika juzi kwenye
Uwanja wa Azam Complex, Nyoso alimfanyia madhambi nahodha wa timu ya
Azam, John Bocco.
Tukio kama hilo liliwahi kufanywa na mchezaji huyo kwa mchezaji wa
Simba, Elius Maguli na TFF ikamfungia mechi nane kwa kumfanyia kitendo
hicho cha udhalilishaji.
Katika kesi hiyo Nyoso ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumfanyia
vitendo vya udhalilishaji adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya
57 na Ibara ya 11 (f) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.
Tukio hili liliripotiwa kutokea juzi lakini mwamuzi hakuona ila
kupitia picha za mnato na kanda za video tukio hilo lilinaswa na
kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Nyoso akifanya tukio la udhalilishaji dhidi ya Elius Maguri msimu uliopita wakati Maguri akicheza kwenye klabu ya Simba SC.
0 comments:
Post a Comment