Mamia ya wafungwa katika Gereza moja
nchini jamuhuri ya Afrika ya kati wametoroka wakati ambapo kumekuwa na
machafuko yaliyosababisha watu kupoteza maisha.
Baada ya Dereva wa
Taxi muumini wa dini ya kiislamu kuuawa, mapigano yalizuka siku ya
jumamosi kati ya wanamgambo wa kikristo na makundi ya kiislamu.
Wafuasi
wa wanamgambo wa kikristo wajulikanao kwa jina anti-balaka
walishambulia gereza siku ya jumatatu, na kuwatorosha mamia ya Wanajeshi
na wanamgambo.
Jamuhuri ya Afrika ya kati imekuwa ikikumbwa na
machafuko tangu kundi la waasi wa kiislamu, Seleka kuchukua madaraka
mwezi Machi mwaka 2013.
Kundi la Seleka baadae liliondolewa madarakani, hali iliyosababisha machafuko.Maelfu ya watu waliyakimbia makazi yao.
Tangu machafuko mapya kuanza wikiendi, zaidi ya watu 30 wameuawa.
Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF limesema watoto watatu waliuawa na mmoja kwa kuchinjwa.
Shirika
la habari la AP limesema Watu 500 wametoroka gereza la Ngaragba
lililopo mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui siku ya jumatatu jioni.
Rais
wa mpito wa nchi hiyo Catherine Samba Panza amelazimika kukatiza safari
yake ya kuelekea kwenye Mkutano mkuu wa umoja wa mataifa.
Uchaguzi wa urais umepangwa kufanyika mwezi Oktoba, mwezi mmoja kabla Baba Mtakatifu Francis kutembelea Bangui.
0 comments:
Post a Comment