Wakati
kampeini zikiendelea kushika kasi,Tume ya uchaguzi nchini imetakiwa kufanya
ziara za kimyakimya katika maeneo zinapofanyika kampeini huzo, ili kubaini
changamoto za vitisho zinazotolewa na baadhi ya wagombea huko vijijini,na
kuchukua hatua za makusudi,ikiwa ni pamoja na kubaini fununu zinazoenezwa juu
ya watu wanaonunua vitambulisho vya kupigia kura,kutoka kwa wananchi
jambo ambalo litawakosesha haki ya kupiga kura.
Rai
hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF) Bibi Magdalena
Sakaya ambaye pia ni mgombea wa jimbo la kaliua mkoani Tabora,wakati
akizungumzia changamoto za kampeini ambazo anakumbana nazo katika jimbo hilo
ambapo amesema kuwa, bila tume kuzunguka wananchi wengi wanaweza wasipige kura.
Suala
la wananchi kupolwa vitambulisho vya mpiga kupigia kura limelalamikiwa na chama
cha mapinduzi katika wilaya ya uyui mkoani humo,ambapo katibu wa chama hicho
Bw.Inocent Namzaba amewataka wananchi kutorubunika kuvilinda kama mboni ya
macho yao,huku mgombea ubunge jimbo la Tabora kasikazini akiwataka
wananchi,kuunga mkono kaurimbiu yake ya siasa ni uchumi.
0 comments:
Post a Comment