Katika
kudumisha hali ya amani na mshikamano uliopo hapa nchini wakati tunapoelekea
kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika hivi karibuni,baadhi ya viongozi wa
madhehebu ya dini mkoani Kagera wamewatahadharisha watanzania kwa kuwataka
wawe makini na wagombea wa nafasi za uongozi ambazo ni pamoja
na urais, ubunge na udiwani ambao wanaoeneza siasa zenye viashiria vya
kuwagawa na kuchochea hali ya uvunjifu wa amani.
Tahadhari
hiyo imetolewa leo kwa nyakati tofauti mjini bukoba na askofu msaidizi wa jimbo
la kanisa katoriki la Bukoba,Methodius Kilaini na katibu mkuu wa baraza la
waislamu (BAKWATA) wa mkoa wa Kagera Bashiru Kaboyo, ambao
wanaelezea athari za siasa za udini, ukabila,chuki na kejeli zinazohubiriwa na
baadhi ya wagombea zinavyohatarisha hali ya amani na mshikamano walionao
watanzania.
Kwa
upande wake katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) katika mkoa wa Kagera,ali ame amesema
chama hicho kwenye kampeni zake kitaendelea kuhuburi amani kwa kuwa amani
inapovurugika inapelekea watu kukimbia nchi yao,naye Victor Sherejei ni
katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) katika manispa
ya bukoba anayetaja mambo ambayo yanaweza kuleta uvunjifu wa amani
hapa nchini,huku augustine ulomi,kamanda wa jeshi la polisi mkoani
Kagera akiwatahadharisha viongozi watakaokiuka sheria za nchi kabla na baada ya
uchaguzi mkuu.
0 comments:
Post a Comment