Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE ameombwa na amekubali kujiunga na kundi la watu mashuhuri duniani wakiwemo viongozi wa Afrika,matajiri wa Marekani na watu wengine mashuhuri katika kutafuta majawabu ya kufuta ugonjwa wa Malaria Duniani kwa kuanzia na Bara la Afrika.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais kwa vyombo vya habari,ombi kwa Rais KIKWETE kujiunga na kundi hilo ambalo litaongozwa na tajiri mkubwa zaidi duniani, BILL GATES, liliwasilishwa kwa mara ya kwanza kwake na Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Malaria, RAY CHAMBERS, tajiri mwingine nchini Marekani.
Wakati huo huo Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE ametoa rai kwa Wabunge wa Bunge la Marekani kufunga masoko ya pembe za ndovu na faru duniani, kama njia yenye uhakika ya kukomesha ujangili dhidi ya wanyamapori katika nchi za Afrika.
Rais KIKWETE ametoa rai hiyo alipohutubia Umoja wa Wabunge wa Bunge la Marekani ambao wanalenga kulinda na kuhifadhi wanyamapori na uhifadhi duniani.
0 comments:
Post a Comment