Image
Image

Uchunguzi uliofanywa na Umoja wa Mataifa wakosoa kushindwa kwa dunia kuwalinda wakimbizi.

Umoja wa Mataifa umesema dunia ilikuwa inawaangusha wakimbizi wa Syria zaidi ya Milioni nne wengi wao wakiwa wamekimbilia nchi jirani za Mashariki ya Kati.
Uchunguzi wa uliofanywa na Umoja huo umekosoa kushindwa kwa dunia kuwalinda wakimbizi wa nchi hiyo na kusema kushindwa huko kumechochea mgogoro wa sasa wa wahamiaji Barani  Ulaya.
Ripoti ya hivi karibuni ya uchunguzi huo inasema Wasiriya 2,000 waliokuwa wanajaribu kwenda Ulaya wamekufa maji katika Bahari ya Kati au Mediterranean.
Zaidi ya wakimbizi Milioni nne wa Syria wako Uturuki, Lebanon, Jordan, Iraq, Misri na Kaskazini mwa Afrika.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment