Image
Image

Uhaba wa miundombinu ya sekta ya Afya walazimu wakazi wa kyela kufuata huduma hiyo umbali wa asilimia 70.


Zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wa wilaya ya Kyela wanapata huduma za afya hususan matibabu katika Hospitali za wilaya za jirani hali inayosababishwa na serikali kutowekeza vya kutosha katika Hospitali za umma wilayani humo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ambao umeandaliwa maalum kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa ubunge na madiwani kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo wilayani Kyela,mgombea ubunge wa jimbo la Kyela,Abrahamu Mwanyamaki amesema wilaya ya Kyela inakabiliwa na changamoto kubwa ya ubovu wa miundombinu ya afya,jambo ambalo linasababisha zaidi ya asilimia 70 ya wananchi wilayani humo kupata huduma za afya katika wilaya za jirani.

Mbunge wa mbeya mjini aliyemaliza muda wake,Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Mr.ii Sugu amesema kutokana na huduma mbovu za Kiafya zinazotolewa na serikali ya chama cha mapinduzi, wananchi wanahitaji mabadiliko ambayo kwa mkoa wa mbeya wenye majimbo 13 ya uchaguzi UKAWA wanauhakika kunyakua majimbo zaidi ya 10.

Baadhi ya viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo wamewataka mahasimu wao kisiasa,kuendesha kampeni za kistaarabu ili kutoa fursa ya wananchi kuisikiliza sera, huku wakidai kuwa wanaimani kubwa na wagombea wao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment