Umati wenye
hasira na vurugu wamekuwa wakiwashambulia mashoga mara kwa mara nchini Kenya
licha ya kuwa waathiriwa wa mashambulizi hayo kupuuzwa na polisi wakipeleka
malalamishi yao katika vituo vya sheria
Ushoga ni mwiko Kenya na karibu nchi zote barani Afrika,mashoga
nchini Kenya hupewa adhabu ya kufungwa kwa muda wa miaka 14.
Limekuwa jambo la kawaida hasa Afrika ya mashariki kuwa na
visa vya ukatili dhidi ya watu wanaodhaniwa kuwa mashoga na hata wakiwasilisha
kesi zao polisi huonyesha kutojali kufuatilia kesi hizo.
Kulingana na ripoti kutoka kwa shirika la kutetea haki za binadamu Kenya HRW,pwani
ya Kenya kumekuwa na zaidi ya matukio 6 mwaka 2008
ya ukatili dhidi ya mashoga.
Mtafiti wa HRW Neela Ghoshal alisema kuwa viongozi wa
kidini wa kikristo na kiislamu wamekuwa mstari wa mbele katika kufanya
uchochezi wa vurugu dhidi ya kundi hilo la watu.
Mnamo mwaka 2014 Uganda na Nigeria
zilipitisha sheria ngumu dhidi ya mashoga ingawa baadaye sheria hiyo
ilipinduliwa.
0 comments:
Post a Comment