Rais
Barack Obama asisitiza katika mkutano na Umoja wa Mataifa juu ya athari za
maendeleo duniani kwa ajili ya njaa,umaskini na vita na kuahidi kuwa atajiunga
nao katika harakati za kufanya maendeleo duniani.
Obama aliongea kuhusu mwongozo mpya wa wa kuondoa njaa na
umaskini duniani kusema kuwa ajenda hiyo mpya ya kuleta maendeleo duniani
itakuwa sio msaada bali ni njia ya uwekezaji bora ambao utaweza kukimu
hali ya baadaye.
Obama alitoa utetezi mkubwa wa ajenda hiyo mpya itakayochukua muda wa
miaka 15 ambao unatarajiwa kupata ufanisi wake wa
matrilioni ya dola kutoka nchi kadhaa,makampuni na asasi za kiraia.
"Vita hutishia maendeleo ya nchi,na vita mara nyingi hutokana na
utawala mbaya,"Obama alisema huku akigusia mgogoro wa wakimbizi mbaya
zaidi kuwahi kutokea katika historia tangu vita vya pili vya dunia.
Viongozi kutoka Ufaransa,Japan na Uturuki
pia walihutubia katika siku ya mwisho ya mkutano wa maendeleo unaofanywa kila
mwaka kwa lengo ya kufanya mjadala wa ngazi za juu na kupa nchi tofauti kupitia
viongozi wao kutoa maoni kwa upana kuhusu kufanya maendeleo duniani.
Hata hivyo taarifa ziliarifu kuwa rais wa Urusi Vladimir Putin
hajaudhuria mkutano huo wa Umoja wa Mataifa kwa muda wa muongo mmoja.
0 comments:
Post a Comment