Kikao cha Kamati ya nidhamu ya TFF kilichokutana ndani ya
saa 72, kimefungia nahodha wa Mbeya City, Juma Said Nyosso kucheza soka kwa
miaka miwili.
Pamoja na miaka hiyo miwili, Nyosso ametozwa faini ya Sh
milioni mbili kutokana na kitendo chake cha kumshika makalio nahodha wa Azam
FC, John Bocco.
Hii ni mara ya pili kwa Nyosso kushiriki katika tukio, mara
ya kwanza alimtomasa Elius Maguli wakati akiichezea Simba.
Kutokana na picha ilivyochapishwa kwenye gazeti la Championi
na SALEHJEMBE akafungiwa kucheza mechi nane.
Baada ya hapo, Nyosso aliwaomba radhi Watanzania pamoja na
wapenda soka wote, lakini bado amerudia.
0 comments:
Post a Comment