Image
Image

Vifo vitokanavyo kuumwa na nyoka kuongezeka baada ya dawa kutibu kuisha.

Shirika la hisani la kimataifa la madaktari wasiokuwa na mipaka limeonya kwamba vifo
vinavyotokana na kuumwa na nyoka huenda vikaongezeka  kwa sababu ya kuisha kwa dawa
inayotibu sumu ya nyoka.
Kwa mujibu wa shirika hilo linalojulikana kifupi kama MSF inakadiriwa kwamba watu laki
moja huuawa na nyoka kila mwaka.
Wataalamu wa shirika hilo wamesema akiba ya dawa iliyopo sasa itamalizika mwezi Juni
mwakani na hakuna mpango maalum wa kuziba pengo lake.
Wamesisitiza kuwa dawa hiyo ya kutibu sumu ya nyoka ijulikanayo kwa jina la Fav-Afrique
ilikuwa muhimu sana hasa kwa nchi za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment