Image
Image

BUHARI asifia jeshi lake kwa kupambana na Boko Haramu.

Rais MUHAMMADU BUHARI wa Nigeria amesifu jeshi lake la ulinzi kwamba limepata mafanikio makubwa katika kupambana na wapiganaji wa kikundi cha Boko Haramu hasa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Mwishoni mwa ziara yake huko Ghana ambako alikutana na Rais wa nchi hiyo Bwana JOHN
DRAMANI MAHAMA kiongozi huyo wa Nigeria amesema malengo ya mjeshi yake ni kuona kwamba  wapiganaji hao hawajiimarishi na kuteka tena miji na vijiji.
Mwezi uliopita Bwana BUHARI aliahidi kuwashinda wapiganaji wa Boko Haram ndani ya miezi mitatu.
Amefahamisha pia kwamba kundi la watu lililotekwa na Boko Haram katika msitu wa Sambisa limegunduliwa lakini bado haijafahamika wazi kama kati ya hao ni wanafunzi wa kike waliotekwa kutoka Chibok mwaka uliopita.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment