Viongozi wa Somalia kwa udhamani wa Mamlaka ya Nchi za Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika - IGAD- wanakutana kujadili hatma ya nchi yao katika kuelekea uchaguzi mwakani.
Kuna vyama vya siasa vipatavyo 18 nchini Somalia na jukumu la kwanza litakuwa kujadili Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyoanzishwa hivi karibuni ambayo baadhi ya mamlaka za mikoa zinaipinga.
Jukumu la Tume hiyo litakuwa kuweka miongozo ambayo itapaswa kuzingatiwa na vyama vya siasa wawakilishi wake kwenye tume hiyo kwa niaba ya wananchi ndiyo watachagua rais, wabunge na madiwani.
Katika mkesha wa mazungumzo yao mjini Mogadishu, mji mkuu wa Somalia Rais HASSAN SHEIKH MOHAMUD anasema anaamini uchaguzi huo wa rais, wabunge na serikali za mitaa hapo mwezi Agosti mwakani utakuwa huru, haki na wazi.
0 comments:
Post a Comment