TATIZO la usafiri katika Jiji la Dar es Salaam linatarajia kupungua
baada ya mabasi 138 ya Mradi wa mabasi Yaendayo Haraka (BRT)
unaotarajiwa kuanza kazi Oktoba 2 mwaka huu kuwasili katika Bandari ya
Dar es Salaam yakitokea China.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki amekuwa mmoja wa
mashuhuda, baada ya kujionea mabasi hayo alipotembelea Bandari ya Dar es
Salaam jana. Akizungumza baada ya kuyaona bandarini Dar es Salaam,
alisema: “Tumefikia hatua nzuri na naipongeza Kampuni ya UDA Rapid
Transit (UDART) kwa kuleta mabasi hayo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma
hii ya usafiri katika kipindi cha mpito.
Hii itasaidia kuondoa adha ya usafiri kwa wakazi wa jiji hili.”
Alisema kampuni hiyo imepewa jukumu la kuendesha kipindi cha mpito ili
waweze kupata uzoefu na zabuni ya mwendesha mradi kipindi cha kudumu
itakapo tangazwa itasaidia wao kushindana.
Aliongeza kuwa, Serikali ilifanya kazi kubwa kuunganisha Kampuni ya
Usafiri Dar es Salaam na wamiliki wa daladala na baadaye kuanzisha
kampuni ya UDART. Aidha alikanusha kuwa nauli za mabasi hayo imepangwa
kuwa Sh 900 zilizotolewa katika mtandao, na kusema huo ni uzushi na
upotoshaji na aliyefanya hivyo anatafutwa ili sheria ichukue mkondo.
Alisema suala la nauli linahusisha ushiriki wa taasisi mbalimbali
chini ya Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) hivyo
uzushi huo umewaletea usumbufu mkubwa wakazi wa Dar es Salaam hivyo
wanatakiwa kuwapuuzia.
Msemaji wa Kampuni ya UDA Rapid Transit (UDA-RT), Sabri Mabrouk
alisema mabasi yote yameingia yakiwemo ya meta 12 yapo 101 na meta 18
yapo 39 na huduma ya usafiri kipindi cha mipito itanza baada ya
kukamilisha taratibu za bandari.
“Tuliahidi kuwa mwezi huu wa tisa mabasi yatakuwa yamewasili na ni
kweli yamekuja,” na kwa pamoja na yale ya kufundishia yatakuwa mabasi
140,” alisema Mabrouk. Alifafanua kwamba mabasi hayo yametokea kiwandani
China na yanakidhi miundombinu ya barabara ya mradi wa BRT kama
walivyokubaliana.
0 comments:
Post a Comment