UJUMBE wa waangalizi 34 wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU),
wamewasili Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa uchaguzi
mkuu.
Waangalizi hao wanaungana na kundi kuu la EU EOM la watathmini wa uchaguzi ambao waliwasili Septemba 11, mwaka huu.
Msafara wa EU EOM nchini Tanzania, utaongozwa na Mbunge wa Bunge la Ulaya kutoka nchini Uholanzi, Judith Sargentini.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana na
Ofisa Habari wa umoja huo hapa nchini, Sarah Fradgley ilisema ujumbe
huo baada ya kupata maelezo kwa siku mbili jijini Dar es Salaam
yanayohusu mchakato mzima wa uchaguzi, waangalizi hao watasambazwa mikoa
yote.
“Waangalizi hawa watasambazwa makundi ya watu wawili wawili, jukumu
lao kwa wiki sita zijazo ni kuangalia maandalizi ya uchaguzi, kampeni na
kazi ya utendaji wa mamlaka husika.
“Wataangalia upigaji kura na kuhesabiwa, uorodheshwaji wa matokeo na
namna ya kushughulikia malalamiko na rufaa zinazoweza kujitokeza.
“Waangalizi wetu watakutana na maofisa wa uchaguzi, wagombea na
wawakilishi wa asasi za kiraia na watatuma ripoti ya watakayoyaona kwa
kundi kuu Dar es Salaam, ili tathmini ya kina na isiyo na upendeleo
iweze kufanyika,”ilisema taarifa hiyo.
EU EOM, imetumwa baada ya kupata mwaliko kutoka Serikali ya
Tanzania,Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar
(ZEC).
Tarifa hiyo, ilisema jukumu la ujumbe huo, ni kuangalia masuala yote
ya mchakato wa uchaguzi na kutathmini kama uchaguzi unazingatia misimamo
ya kimataifa na ya kikanda kuhusu chaguzi za kidemokrasia.
Mwangalizi mkuu, Sargentini, atawasili nchini keshokutwa na atakutana na waandishi wa habari Septemba 30, mwaka
0 comments:
Post a Comment