SIKU moja baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod
Slaa kudai mgombea urais wa chama hicho/Ukawa, Edward Lowassa hafai
kuwania nafasi hiyo Vijana ambao inaaminiwa kuwa siwa na chama halali wa Chadema wameibuka jijini Dar es Salaam huku
wakitishiana kwa mapanga.
Ilidaiwa kuwa walichukua hatua hiyo kutokana kupishana kauli kwa
kutoridhishwa na kitendo cha Dk. Slaa kuachia ngazi ndani ya chama hicho
ambacho alikitumikia kwa nguvu zake zote,lakini wachache ndiyo
wanafaidi matunda yake.
Kutokana na hali hiyo, hali ya usalama ilikuwa si shwari katika ofisi
za makao makuu ya Chadema zilizopo Mtaa wa Ufipa, Kinondoni, ambapo
walinzi wa chama ilibidi kutoa silaha, yakiwemo mapanga ili kujilinda
dhidi ya wapenzi hao wa. Dk Slaa.
Wapenzi hao FEKI wa Dk. Slaa waliandamana wakishinikiza chama hicho
kumrudisha madarakani huku wakitoa amri ya kutaka kiachane na mgombea wake
wa urais, Lowassa kwani baada ya kuingia Chadema kumekuwa na mpasuko
mkubwa.
Tafrani hiyo ilitokea saa sita mchana baada ya kundi la watu
waliojitambulisha kama wapenzi na wanachama wa Chadema kukusanyika eneo
la Kinondoni Morocco wakiimba nyimbo za “tunamtaka Babu, hatumtaki
Mamvi” (wakimaanisha wanamtaka Slaa na hawamtaki Lowassa).
Ilidaiwa kuwa vijana hao walitoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es
Salaam na idadi yao inazidi 100.
Vijana hao walikuwa wamevaa mavazi ya
chama hicho huku wakiwa na mabango pamoja na bendera za Chadema.
Pia,vijana hao wa kiume na kike wakati wakisubiriana na kutafuta
namna ya kupeleka malalamiko yao kwenye chama walisikika wakiimba nyimbo
huku wakihamasishana kwa maneno ya “Peoples Power”.
Kutokana na hali hiyo Jeshi la Polisi liliingilia kati na kuzuia
maandamano hayo kwa kufyatua mabomu ya machozi na baada ya purukushani
ya muda mfupi, liliwakamata vijana waliohusika katika mkusanyiko huo
kwani ilikuwa ni kinyume cha sheria.
Pamoja na askari kufika hawakusikiliza agizo la Polisi na badala yake
waliamua kwenda Makao Makuu ya Chadema kueleza malalamiko yao kwamba
Dk. Slaa ameonewa na chama kinatakiwa kimrudishe katika nafasi yake
vinginevyo hawataelewa chochote.
Mwandishi wa gazeti hili ambaye alifuatilia sakata hilo hadi ofisi za
Chadema, alikuta vijana wa chama hicho wakianza kuingia na kujaa kwa
wingi katika nje ya ofisi za chama.
Mmoja wa vijana hao alisikika akiwaambia wenzake kuwa wamepewa
taarifa kuwa kundi hilo linaloandamana limetumwa kwenda kufanya fujo na
kwamba wao wanatakiwa kujiandaa na kukilinda chama kwa gharama yoyote.
Dakika chache baada ya kundi la Morocco kufika Mtaa wa Ufipa yalipo
Makao Makuu ya Chadema, vijana walinzi walianza kutoa silaha kama
mapanga na kuwatisha vijana hao.
Kulikuwa na kubadilishana lugha kwa dakika chache baina ya pande hizo
mbili lakini baada ya muda mfupi mawe yalianza kurushwa huku watu
kutoka Morocco wakikimbia na kuondoka eneo hilo.
Kutokana na hali tete eneo hilo, eneo la Kinondoni hususan Mtaa wa
Ufipa na Togo walionekana askari Polisi na wenye maduka na nyumba
walianza kuingiwa na taharuki.
Baada ya vijana hao kuondoka Makao Makuu ya Chadema,walinzi wa chama
hicho walianza kuzunguka katika mitaa ya jirani na ofisi zao na
kukamata mtu yeyote waliyekuwa hawamfahamu.
Kutokana na hali hiyo, gazeti hili liliwasiliana jana na Jeshi la
Polisi Kinondoni na kujulishwa kuwa linawashikilia vijana 10
wanaosadikiwa kuhusika na maandamano yaliyofanyika katika eneo la
Morocco jijini Dar es Salaam ili kuwahoji.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,
Camilius Wambura alisema vijana hao wanaendelea kuhojiwa ili kujua ni
kwa namna gani wameshiriki maandamano hayo.
Wambura alisema mahojiano
hayo yanaweza kuchukua wiki moja au zaidi.
Kamanda Wambura alisema baada ya vijana hao kuandamana walitawanywa
na Jeshi la Polisi kwa kutumia mabomu ya machozi ambapo baadhi walitupa
mabango waliyokuwa nayo barabarani na kukimbia lakini wengine
walikamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay.
Alisema baadhi walishikiliwa katika ofisi za Makao Makuu ya Chadema
zilizopo eneo la Kijitonyama, wengine Ofisi za Mtengaji Kata maeneo ya
Biafra na wengiene eneo hilo la Morocco na jumla ya vijana hao ni 10.
Ilivyokuwa
Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliandamana kupinga hatua ya Dk. Slaa
kustaafu siasa kutokana na ujio wa Lowassa kwenye chama hicho. Wafuasi
hao waliokuwa na mabango mbalimbali yaliyokuwa na picha za Dk. Slaa
yenye jumbe tofauti tofauti waliandamana jana maeneo ya Morocco, Mwenge.
Wakati wa maandamano hayo wafuasi hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali ikiwemo ya kuwa”hatumtaki Lowassa…hatumtaki Lowassa”.
Mashuhuda
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili baadhi ya mashuhuda
walioshuhudia tukio hilo walisema wao walishangaa kuona watu waliokuwa
wamebeba mabango wakipita huku wakiimba barabarani ambapo baada ya
kuwauliza ni nini kinaendelea hawakupewa jibu lolote.
Rashid Said alisema wakati maandamano hayo yakiendelea walitokea
askari waliokuwa na gari aina ya Defender tatu na kuanza kupiga mabomu
ya machozi hali iliyowasababishia wafuasi hao kutawanyika.
Alisema baadhi wafuasi hao walitawanyika na wengine kukimbia lakini baadhi yao walikamatwa.
Said alisema baada ya muda mfupi alishuhudia wengine wakiachiwa baada ya
ndugu zao kwenda kuulizia katika kituo hicho chanzo cha kukamatwa kwa
ndugu zao.
Gazeti hili lilishuhudia baadhi ya wafuasi walioachiwa wakitembea
kando ya barabara huku wakilalamika kuwa kwa nini wakamatwe wakati
wameandamana kutafuta haki yao.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment