Image
Image

Msanii wa Kenya afariki visiwa vya Mbudya Dar.

MSANII wa muziki wa genge nchini Kenya, Simon Njoroge ‘Shreekezy’, amepoteza maisha akiwa jijini Dar es Salaam katika visiwa vya Mbudya vilivyopo Bahari ya Hindi.
Msanii huyo anadaiwa kufariki Agosti 30 baada ya boti aliyokuwa akiiendesha baharini akitokea Hoteli ya Whitesands kuelekea visiwa hivyo kumtupa ambapo alifariki dunia na mwili wake ulipatikana baada ya siku tatu.
Msanii huyo alikuwa nchini Tanzania kwa siku nane kabla ya kifo chake kutokea. Hata hivyo, inadaiwa katika boti hiyo alikuwa na mwanamke wa kizungu ambaye alishindwa kumuokoa wakati wa ajali hiyo ilipowatokea.
Msanii huyo mwaka 2011 aliwania tuzo ya msanii mwenye kipaji nchini Kenya katika tuzo za Chaguo la Teeniez.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment