Wakizungumza wakati wa Harambee ya kutafuta fedha
kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu
ya Madarasa,Vyoo na Nyumba za walimu katika shule hizo,baadhi ya walimu
wakiwemo walimu wakuu wa shule hizo,wamesema upungufu huo mkubwa wa vyumba vya madarasa na
miundombinu mingine ya shule imekuwa ikisababisha
wanafunzi kusoma katika mazingira magumu hasa wakati wa mvua na jua kali.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kiriba
Bw.Semeni Mkama,akizungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho,amesema
uongozi wa kijiji utalazimika sasa
kutunga sheria ndogondogo kwa ajili kusaidia ukusanyaji wa michango
kutoka kwa wananchi ili kuwezesha
upatikanaji wa haraka wa fedha za ukarabati na ujenzi wa miundominu hiyo ya elimu katika shule hizo
na hivyo kuwandolea adha mhiyo kubwa
wanayoipata wanafunzi na walimu wao.
Kiasi cha zaidi shilingi milioni 44.8 kinahitajika
kwa ajili ya ukarabati na ujenzi huo wa
miondombinu katika shule hizo huku harambea hiyo ikifanikiwa kukusanya fedha taslimu na vifaa vya ujenzi
vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 8.7.Bofya hapo kuona zaidi->http://www.itv.co.tz



0 comments:
Post a Comment