Image
Image

Lowassa asema amejipanga kikamilifu kwa kutumia sera zilizopo akiingia ikulu kumaliza kero za wananchi.

Mgombea urais wa UKAWA Mh.Edward Lowasa amefanya mikutano ya kampeni katika  majimbo matano ya mikoa ya Kigoma na Tabora na kuwawaomba wananchiwa maeneo hayo kuungana na watanzania wengine wanaopenda mabadiliko kumchagua rais,wabunge na madiwani wa vyama vya UKAWA ili kurahisisha kazi ya kuondoa kero zinazowakabili.
Akizungumza katika mikutano hiyo Mh.Lowasa amesema kazi ya kukabiliana na changamoto zinazoandamana wananchi kwa muda  mrefu iko ndani ya uwezo wake na viongozi wenzake wa ukawa na itakuwa  nyepesi  zaidi kama  wananchi  watatoa  ushirikiano.
Mh.Lowassa ambaye ameweza kuwafikia wananchi wengi wa vijijini baada ya kuanza kutumia HELCOPTER amesema UKAWA imejipanga kikamilifu na kutumia sera zilizoko kwenye ilani ya kutatua kero nyingi zinazowakabili wananchi kinaachotakiwa  sasa ni ushirikiano wa wananchi.
Viongozi na makada wengine wa UKAWA walioambatana  na mgombea wamewaomba  wananchi kuwachagua viongozi wa UKAWA wakiwemo madiwani  na waabunge  ili kutimiza lengo la mabadiliko.
Mh.Lowassa anaendelea na kampeni katika majimbo ya mkoa wa Tabora na baadaye  Shinyanga.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment